Methali 19:10-12
Methali 19:10-12 BHN
Haifai kwa mpumbavu kuishi kwa anasa, tena ni vibaya zaidi mtumwa kuwatawala wakuu. Mwenye busara hakasiriki upesi; kusamehe makosa ni fahari kwake. Ghadhabu ya mfalme ni kama ngurumo ya simba, lakini wema wake ni kama umande juu ya majani.