Methali 19:10-12
Methali 19:10-12 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Maisha ya anasa hayampasi mpumbavu; Sembuse mtumwa awatawale wakuu. Busara ya mtu huiahirisha hasira yake; Nayo ni fahari yake kusamehe makosa. Ghadhabu ya mfalme ni kama ngurumo ya simba; Bali hisani yake kama umande juu ya majani.
Methali 19:10-12 Biblia Habari Njema (BHN)
Haifai kwa mpumbavu kuishi kwa anasa, tena ni vibaya zaidi mtumwa kuwatawala wakuu. Mwenye busara hakasiriki upesi; kusamehe makosa ni fahari kwake. Ghadhabu ya mfalme ni kama ngurumo ya simba, lakini wema wake ni kama umande juu ya majani.
Methali 19:10-12 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Maisha ya anasa hayampasi mpumbavu; Sembuse mtumwa awatawale wakuu. Busara ya mtu huiahirisha hasira yake; Nayo ni fahari yake kusamehe makosa. Ghadhabu ya mfalme ni kama ngurumo ya simba; Bali hisani yake kama umande juu ya majani.
Methali 19:10-12 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Maisha ya anasa hayampasi mpumbavu; Sembuse mtumwa awatawale wakuu. Busara ya mtu huiahirisha hasira yake; Nayo ni fahari yake kusamehe makosa. Ghadhabu ya mfalme ni kama ngurumo ya simba; Bali hisani yake kama umande juu ya majani.
Methali 19:10-12 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Haistahili mpumbavu kuishi katika anasa, itakuwa vibaya kiasi gani kwa mtumwa kuwatawala wakuu. Hekima ya mtu humpa uvumilivu, ni kwa utukufu wake kusamehe makosa. Ghadhabu ya mfalme ni kama mngurumo wa simba, bali wema wake ni kama umande juu ya nyasi.