Isaya 40:9-10
Isaya 40:9-10 BHN
Nenda juu ya mlima mrefu, ewe Siyoni, ukatangaze habari njema. Paza sauti yako kwa nguvu, ewe Yerusalemu, ukatangaze habari njema. paza sauti yako bila kuogopa. Iambie miji ya Yuda: “Mungu wenu anakuja.” Bwana Mungu anakuja na nguvu, kwa mkono wake anatawala. Zawadi yake iko pamoja naye, na tuzo lake analo.


