Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Isaya 40:9-10 - Compare All Versions

Isaya 40:9-10 BHN (Biblia Habari Njema)

Nenda juu ya mlima mrefu, ewe Siyoni, ukatangaze habari njema. Paza sauti yako kwa nguvu, ewe Yerusalemu, ukatangaze habari njema. paza sauti yako bila kuogopa. Iambie miji ya Yuda: “Mungu wenu anakuja.” Bwana Mungu anakuja na nguvu, kwa mkono wake anatawala. Zawadi yake iko pamoja naye, na tuzo lake analo.

Shirikisha
Isaya 40 BHN

Isaya 40:9-10 SRUV (Swahili Revised Union Version)

Wewe uuhubiriye Sayuni habari njema, Panda juu ya mlima mrefu; Wewe uuhubiriye Yerusalemu habari njema, Paza sauti kwa nguvu; Paza sauti yako, usiogope; Iambie miji ya Yuda, Tazameni, Mungu wenu. Tazameni, Bwana Mungu atakuja kama shujaa, Na mkono wake ndio utakaomtawalia; Tazameni, thawabu yake i pamoja naye, Na fidia yake i mbele zake.

Shirikisha
Isaya 40 SRUV

Isaya 40:9-10 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)

Wewe uuhubiriye Sayuni habari njema, Panda juu ya mlima mrefu; Wewe uuhubiriye Yerusalemu habari njema, Paza sauti kwa nguvu; Paza sauti yako, usiogope; Iambie miji ya Yuda, Tazameni, Mungu wenu. Tazameni, Bwana Mungu atakuja kama shujaa, Na mkono wake ndio utakaomtawalia; Tazameni, thawabu yake i pamoja naye, Na ijara yake i mbele zake.

Shirikisha
Isaya 40 SUV

Isaya 40:9-10 NEN (Neno)

Wewe uletaye habari njema Sayuni, panda juu ya mlima mrefu. Wewe uletaye habari njema Yerusalemu, paza sauti yako, piga kelele kwa nguvu, paza sauti, usiogope; iambie miji ya Yuda, “Yuko hapa Mungu wenu!” Tazameni, BWANA Mwenyezi anakuja na nguvu, nao mkono wake ndio utawalao kwa ajili yake. Tazameni, ujira wake u pamoja naye, nayo malipo yake yanafuatana naye.

Shirikisha
Isaya 40 NEN