Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Waroma 12

12
Kumtumikia Mungu kwa Kweli.
1*Nawaonya, ndugu, kwa hivyo, Mungu alivyowaonea uchungu, mtoe miili yenu, iwe vipaji vitakatifu vya tambiko vyenye uzima vya kumpendeza Mungu; huko ndiko kumtumikia Mungu kunakoelekea.#Rom. 6:13; Yoh. 4:24; 1 Petr. 2:5. 2Msijifananishe nao walio wa siku hizi tu, ila mgeuke, mpewe mawazo mapya, mpate kuyapambanua, Mungu ayatakayo kwamba: Ni mema ya kumpendeza hapo, yatakapotimilika.#Ef. 4:23; 5:10,17.
3Kwa kipaji, nilichogawiwa, namwambia kila mmoja wa kwenu, asiwaze makuu yanayopapita hapo panapopasa kuwaza. Ila awaze, jinsi atakavyopata kuerevuka, kila mtu, kama Mungu alivyomgawia kumtegemea.#Mat. 20:26; 1 Kor. 12:11; Ef. 4:7. 4Kwani ni vivyo hivy: tunavyo viungo vingi katika mwili mmoja, lakini viungo vyote havina kazi moja.#1 Kor. 12:12. 5Vivyo sisi tulio wengi tu mwili mmoja, kwa maana tu wa Kristo, tena kila mmoja na mwenzake tu viungo tu.#1 Kor. 12:27; Ef. 4:25. 6Tena vipaji, tulivyopewa ni vingi, kila mtu anacho chake, kama alivyogawiwa.*#1 Kor. 12:4.
*Mwenye ufumbuaji sharti aupatanishe na kumtegemea Mungu. 7Mwenye utumishi sharti atumike kweli! Mfunzi na aushike ufundisho wake!#1 Petr. 4:10-11. 8Mwenye kuonya sharti aonyeke! Mwenye kugawia sharti anyenyekee! Aliye mkuu sharti ajihimize! Mwenye kutunza wengine sharti avifurahie!#Mat. 6:3; Luk. 14:12; 2 Kor. 8:2; 9:7. 9Mapendano yasiwe ya uwongo! Yachukieni yaliyo mabaya mkigandamiana nayo yaliyo mema!#Amo. 5:15; 1 Tim. 1:5. 10Mpendane kindugu kwa mioyo, tena mwongozane na kuheshimiana ninyi kwa ninyi!#Yoh. 13:4-15; Fil. 2:3; 2 Petr. 1:7. 11Msilegee, panapotakwa wenye kujikaza! Roho zenu ziwe zenye moto mnapomtumikia Bwana!#Ufu. 3:15. 12Furahini, ya kwamba mnacho kingojeo! Yavumilieni maumivu! Fulizeni kuomba!#1 Tes. 5:17. 13Changeni bia, mwapatie watakatifu, wanavyovikosa! Wageni wapokeeni pasipo kunung'unika!#Ebr. 13:2; 3 Yoh. 5-8. 14Changeni bia, mwapatie watakatifu, wanavyovikosa! Wageni wapokeeni pasipo kunung'unika!#Mat. 5:44; Tume. 7:59; 1 Kor. 4:12. 15Furahini pamoja nao wafurahio! Lieni pamoja nao waliao!#Sh. 35:13. 16Mioyo yenu nyote sharti iwe mmoja! Msiyatunukie yaliyo makuu, ila yaliyo manyonge, mfuatane nayo! Msijiwazie wenyewe kuwa wenye akili!*#Rom. 15:5; Fano. 3:7.
Lipizi linalofaa.
17*Msimlipe mtu maovu kwa maovu! Yawazeni yaliyo mazuri mbele ya watu wote!#Yes. 5:21; 1 Tes. 5:15. 18Kwa hivyo, mlivyo, mwe wenye kupatana na watu wote, ikiwezekana!#Mar. 9:50; Ebr. 12:14. 19Wapendwa, msijilipize wenyewe, ila jitengeni, makali (ya Mungu) yapate kutokea! Kwani imeandikwa: Bwana anasema:
Lipizi ni langu mimi, ni mimi nitakayelipisha.
# 3 Mose 19:18; 5 Mose 32:35; Mat. 5:38-44. 20Lakini mchukivu wako akiwa ana njaa, mpe chakula!
Akiwa ana kiu, mpe cha kunywa!
Kwani ukivifanya hivyo,
utampalia makaa ya moto kichwani pake.#Fano. 25:21-22; Mat. 5:44. 21Usishindwe nayo yaliyo maovu, ila maovu uyashinde kwa mema!*

Iliyochaguliwa sasa

Waroma 12: SRB37

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia