Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mateo 8

8
Mwenye ukoma.
(1-4: Mar. 1:40-44; Luk. 5:12-14.)
1*Alipotelemka mlimani, makundi mengi ya watu wakamfuata. 2Mara akaja mwenye ukoma, akamwangukia akisema: Bwana, ukitaka waweza kunitakasa. 3Ndipo, Yesu aliponyosha mkono, akamgusa akisema: Nataka, utakaswe. Mara ukoma ukatakaswa. 4Kisha Yesu akamwambia: Tazama, usimwambie mtu! Ila uende, ujionyeshe kwa mtambikaji, ukitoe kipaji, Mose alichokiagiza, kije kinishuhudie kwao.#Mat. 9:30; Mar. 7:36; Luk. 17:14; 3 Mose 14:2-32.
Mkubwa wa Kapernaumu.
(5-13: Luk. 7:1-10.)
5Yesu alipoingia Kapernaumu, mkubwa wa askari akamjia, akambembeleza akisema: 6Bwana, mtoto wangu amelala nyumbani, anaumia vibaya kwa kulemaa. 7Yesu akamwambia: Mimi ninakuja kumponya 8Lakini yule mkubwa wa askari akamjibu akisema: Bwana, hainipasi, uingie kijumbani mwangu, ila sema neno tu! ndipo, mtoto wangu atakapopona! 9Kwani nami ni mtu wa serikali, ninao askari chini yangu. Nami nikimwambia huyu: Nenda! basi, huenda; na mwingine: Njoo! huja; nikimwagiza mtumishi wangu: Vifanye hivi! huvifanya. 10Yesu alipoyasikia akastaajabu, akawaambia waliomfuata: Kweli nawaambiani: Kwa Waisiraeli sijaona bado mtu mwenye kunitegemea kama huyu.#Mat. 15:28. 11Lakini nawaambiani: Wengi watatoka maawioni na machweoni kwa jua, watakaa chakulani pamoja na Aburahamu na Isaka na Yakobo katika ufalme wa mbingu,#Yes. 49:12; Luk. 13:28-29. 12lakini wana wa huo ufalme watatupwa penye giza lililoko nje; ndiko, kitakakokuwa kilio na kukereza meno.#Mat. 22:13; 24:51; 25:30. 13Kisha Yesu akamwambia mkubwa wa askari: Nenda kwenu, na uyapate uliyoyategemea! Saa ileile mtoto wake akapona.*#Mat. 9:29; 15:28.
Mkwewe Petero.
(14-17: Mar. 1:29-34; Luk. 4:38-41.)
14Ikawa, Yesu alipoingia nyumbani mwa Petero, akamwona mama ya mkewe Petero, amelala kwa kuwa na homa.#1 Kor. 9:5. 15Alipomgusa mkono, homa ikamwacha, akainuka, akamtumikia. 16Ilipokuwa jioni, wakampelekea wengi waliopagawa na pepo; naye akawafukuza pepo kwa neno tu. Nao wote waliokuwa hawawezi akawaponya, 17kusudi litimizwe lililosemwa na mfumbuaji Yesaya:
Yeye ameyachukua manyonge yetu, akajitwisha maumivu yetu.#Yes. 53:4.
(18-22: Luk. 9:57-60.)
18Lakini Yesu alipoona, watu wengi wakimzunguka, akaagiza, wavuke kwenda ng'ambo.#Mar. 4:35; Luk. 8:22. 19Ndipo, mwandishi mmoja alipomjia, akamwambia: Mfunzi, nitakufuata po pote, utakapokwenda. 20Yesu akamwambia: Mbweha wanayo mapango, nao ndege wa angani wanavyo vituo, lakini Mwana wa mtu hana pa kukilazia kichwa chake.#2 Kor. 8:9. 21Mwanafunzi wake mwingine akamwambia: Bwana, nipe ruhusa, kwanza niende, nimzike baba yangu!#1 Fal. 19:20. 22Yesu akamwambia: Nifuata mimi, waache wafu, wazikane wao kwa wao!#Mat. 10:37; Fil. 3:13.
Upepo wa baharini.
(23-27: Mar. 4:36-41; Luk. 8:23-25.)
23*Alipoingia chomboni, wanafunzi wake wakafuatana naye. 24Mara kukawa na msukosuko mkubwa baharini, hata chombo kilifunikizwa na mawimbi, lakini yeye alikuwa amelala usingizi. 25Ndipo, walipomjia, wakamwamsha wakisema: Bwana, tuokoe, tunaangamia! 26Yesu akawaambia: Mbona mnaogopa hivyo? Mbona mnanitegemea kidogo tu? Kisha akainuka, akaukaripia upepo na bahari, kukawa kimya kabisa.#Mat. 14:31; 16:8; Sh. 107:23-31. 27Lakini watu wakastaajabu wakisema: Ni mtu gani huyu, ya kuwa hata upepo na bahari zinamtii?*
Wenye pepo kwa Wagadara.
(28-34: Mar. 5:1-17; Luk. 8:26-37.)
28Alipofika ng'ambo katika nchi ya Wagadara, watu wawili waliopagawa na pepo wakakutana naye wakitoka penye makaburi, ni wakorofi mno; kwa hiyo mtu hakuweza kuipita njia ile. 29Mara wakapiga kelele wakisema: Tuko na jambo gani sisi na wewe, mwana wa Mungu? Umejia hapa kutuumiza, siku zetu zikiwa hazijatimia bado?#Luk. 4:41; 2 Petr. 2:4. 30Mbali yao kulikuwako kundi la nguruwe wengi waliokuwako malishoni. 31Wale pepo wakambembeleza wakisema: Ukitufukuza, tutume, tuliingie lile kundi la nguruwe! 32Yesu alipowaambia: Haya! Nendeni! ndipo, pepo walipowatoka, wakawaingia nguruwe. Mara kundi lote likatelemka mbio mwambani, wakaingia baharini, wakafa majini; 33lakini wachungaji wakakimbia, wakaenda zao mjini, wakayatangaza yote, hata mambo ya wenye pepo. 34Mara watu wa mji wakatoka wote, wakutane na Yesu. Walipomwona wakambembeleza, atoke mipakani kwao.

Iliyochaguliwa sasa

Mateo 8: SRB37

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia