Zab 41:7-10
Zab 41:7-10 SUV
Wote wanaonichukia wananinong’ona, Wananiwazia mabaya. Neno la kisirani limemgandama, Na iwapo amelala hatasimama tena. Msiri wangu tena niliyemtumaini, Aliyekula chakula changu, Ameniinulia kisigino chake. Lakini Wewe, BWANA, unifadhili, Uniinue nipate kuwalipa.





