Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Tito 3

3
Dumisha matendo mema
1 # 1 Pet 2:13 Uwakumbushe watu kunyenyekea kwa watawala na wenye mamlaka, na kutii, na kuwa tayari kwa kila kazi njema; 2#Flp 4:5 wasimtukane mtu yeyote, wasiwe wagomvi, wawe wema, wakiwa wapole sana kwa watu wote. 3#1 Kor 6:11; Efe 2:2; 5:8 Maana hapo zamani sisi nasi tulikuwa hatuna akili, tulikuwa waasi, tumedanganywa, huku tukitumikia tamaa na anasa za namna nyingi, tukiishi katika uovu na husuda, tukichukiza na kuchukiana. 4#Tit 2:11; Mit 8:31 Lakini wema wake Mungu Mwokozi wetu, na upendo wake kwa wanadamu, ulipofunuliwa, alituokoa; 5#Efe 2:8,9; 5:26; Yn 3:5; 2 Tim 1:9 si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa mara ya pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu; 6#Yoe 2:28 ambaye alitumwagia kwa wingi, kwa njia ya Yesu Kristo Mwokozi wetu; 7#Rum 3:24 ili tukihesabiwa haki kwa neema yake, tupate kufanywa warithi wa uzima wa milele, kama lilivyo tumaini letu. 8Ni neno la kuaminiwa; na mambo hayo nataka uyasisitizie sana, ili wale waliomwamini Mungu wakumbuke kudumu katika matendo mema. Mambo hayo ni mazuri sana, tena yana manufaa kwa wanadamu. 9#1 Tim 4:7 Lakini ujiepushe na mabishano ya kipumbavu, nasaba, magomvi, na mabishano ya sheria. Kwa kuwa hayana manufaa, tena hayafai kitu. 10#2 Yoh 1:10; Mt 18:15,16 Mtu aliye mzushi, baada ya kumwonya mara ya kwanza na mara ya pili, tengana naye; 11#1 Tim 6:4,5 maana unajua ya kuwa mtu kama huyo ni mpotovu na mtenda dhambi, naye amejihukumia hatia yeye mwenyewe.
Ujumbe wa mwisho na baraka
12 # 2 Tim 4:12 Wakati nitakapomtuma Artema kwako au Tikiko, jitahidi uwezavyo kujiunga nami katika Nikopoli; kwa kuwa nimekusudia kukaa huku wakati wa baridi. 13#Mdo 18:24; 1 Kor 3:5,6 Jaribu uwezavyo kumsaidia Zena, yule mwanasheria, na Apolo, ili wakiwa safarini wasipungukiwe na chochote. 14#Tit 2:14; Mt 7:19; Efe 4:28,29 Watu wetu nao wajifunze kudumu katika matendo mema, kwa matumizi yaliyo lazima, ili wasiwe hawana matunda.
15Watu wote walio pamoja nami wanakusalimu. Tusalimie wale watupendao katika imani.
Neema na iwe pamoja nanyi nyote.

Iliyochaguliwa sasa

Tito 3: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha