Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Tito 2

2
Toa mafundisho mema
1 # 1 Tim 6:3; 2 Tim 1:13 Lakini wewe, nena mambo yanayoambatana na mafundisho mema; 2#1 Tim 5:1 ya kwamba wazee wawe wenye kiasi, wastahivu, wenye busara, wazima katika imani na katika upendo na katika subira. 3#1 Tim 3:11 Vivyo hivyo na wazee wa kike wawe na mwenendo wa utakatifu; wasiwe wasingiziaji, wasiwe wenye kutumia mvinyo nyingi, bali wanaofundisha yaliyo mema; 4ili wawatie wanawake vijana akili, wawapende waume zao, na kuwapenda watoto wao; 5#Efe 5:22 na kuwa wenye kiasi, kuwa safi, kufanya kazi nyumbani mwao, kuwa wema, kuwatii waume zao wenyewe; ili neno la Mungu lisitukanwe.
6Vivyo hivyo na vijana waume uwaonye kuwa na kiasi; 7#1 Tim 4:12; 1 Pet 5:3 katika mambo yote ukijionesha wewe mwenyewe kuwa kielelezo cha matendo mema, na katika mafundisho yako ukionesha usahihi na ustahivu, 8#1 Pet 2:15 na maneno yafaayo yasiyoweza kuhukumiwa makosa, ili yule mwenye kupinga atahayarike, kwa kuwa hana neno baya la kunena juu yetu.
9 # Efe 6:5; 1 Tim 6:1; 1 Pet 2:18 Watumwa na wawatii bwana zao, wakiwapendeza katika mambo yote; wasiwe wakaidi, 10#Tit 1:3 wasiwe wezi; bali wauoneshe uaminifu mwema wote, ili wayapambe mafundisho ya Mungu aliye Mwokozi wetu katika mambo yote. 11Maana neema ya Mungu iwaokoao wanadamu wote imefunuliwa; 12#Efe 1:4; 1 Yoh 2:16 nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa; 13#1 Kor 1:7; Rum 5:2; Flp 3:20 tukilitazamia tumaini lenye baraka na kufunuliwa kwa utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu; 14#Kut 19:5; Kum 4:20; 7:6; 14:2; Zab 130:8; 1 Pet 2:9; 3:13; Gal 1:4; 1 Tim 2:6; Efe 2:10; Eze 37:23 ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wake mwenyewe walio na bidii katika matendo mema.
15 # 1 Tim 4:12 Nena mambo hayo, onya na kukaripia kwa mamlaka yote; asikudharau mtu awaye yote.

Iliyochaguliwa sasa

Tito 2: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha