Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Warumi 16

16
Salamu zake Paulo binafsi
1Namkabidhi kwenu Fibi, dada yetu, aliye mhudumu wa kanisa lililoko Kenkrea; 2ili mmpokee katika Bwana, kama iwapasavyo watakatifu; mkamsaidie katika neno lolote atakalohitaji kwenu; kwa sababu yeye naye amekuwa msaidizi wa watu wengi, akanisaidia mimi pia.
3 # Mdo 18:2,18,26 Nisalimieni Priska na Akila, watenda kazi pamoja nami katika Kristo Yesu; 4waliokuwa tayari hata kukatwa kichwa kwa ajili ya maisha yangu; ambao ninawashukuru, wala si mimi tu, ila na makanisa ya Mataifa yote pia; nisalimieni na kanisa lililomo katika nyumba yao. 5#1 Kor 16:15,19 Nisalimieni Epaineto, mpenzi wangu, aliye malimbuko ya Asia kwa Kristo. 6Nisalimieni Mariamu, aliyejishughulisha sana kwa ajili yenu. 7#2 Kor 8:23 Nisalimieni Androniko na Yunia, jamaa zangu, waliofungwa pamoja nami, ambao ni maarufu miongoni mwa mitume; nao walikuwa katika Kristo kabla yangu. 8Nisalimieni Ampliato, mpenzi wangu katika Bwana. 9Nisalimieni Urbano, mtenda kazi pamoja nami katika Kristo, na Stakisi, mpenzi wangu. 10Nisalimieni Apele, mwenye kukubaliwa katika Kristo. Nisalimieni watu wa nyumbani mwa Aristobulo. 11Nisalimieni Herodioni, jamaa yangu. Nisalimieni watu wa nyumbani mwa Narkiso, walio katika Bwana. 12Nisalimieni Trifaina na Trifosa, wenye bidii katika Bwana. Nisalimieni Persisi, mpendwa aliyejitahidi sana katika Bwana. 13#Mk 15:21 Nisalimieni Rufo, mteule katika Bwana, na mamaye, aliye mama yangu pia. 14Nisalimieni Asinkrito, Flegoni, Herme, Patroba, Herma, na ndugu walio pamoja nao. 15Nisalimieni Filologo na Yulia, Nerea na dada yake, na Olimpa, na watakatifu wote walio pamoja nao. 16#1 Kor 16:20; 1 Pet 5:14 Salimianeni kwa busu takatifu. Makanisa yote ya Kristo yawasalimu.
Maagizo ya mwisho
17 # Mt 7:15; Tit 3:10 Ndugu zangu, nawasihi, waangalieni wale wafanyao fitina na mambo ya kukwaza kinyume cha mafundisho mliyojifunza; mkajiepushe nao. 18#Flp 3:19; Eze 13:18; Kol 2:4; 2 Pet 2:3 Kwa sababu walio hivyo hawamtumikii Bwana wetu Kristo, bali matumbo yao wenyewe; na kwa maneno laini na ya kujipendekeza waidanganya mioyo ya watu wanyofu. 19#Rum 1:8; Mt 10:16; 1 Kor 14:20 Maana utii wenu umewafikia watu wote; basi nafurahi kwa ajili yenu, lakini nataka ninyi kuwa wenye hekima katika mambo mema, na wasio na hatia katika mambo mabaya. 20#Rum 15:33; Mwa 3:15 Naye Mungu wa amani atamponda Shetani chini ya miguu yenu upesi.
Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi. [Amina.]
21 # Mdo 16:1; 19:22; 20:4; Flp 2:19 Timotheo, mtenda kazi pamoja nami, awasalimu, na Lukio, na Yasoni, na Sosipatro, jamaa zangu. 22Mimi Tertio, niliyeandika waraka huu, nawasalimu katika Bwana. 23#Mdo 19:29; 1 Kor 1:14; 2 Tim 4:20 Gayo, mwenyeji wangu, na wa kanisa lote pia, awasalimu. Erasto, wakili wa mji, na Kwarto, ndugu yetu, wanawasalimu.
[ 24Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi nyote. Amina.]
Sifa kwa Mungu
25 # Efe 1:9; 3:5,9; Kol 1:26 Sasa na atukuzwe yeye awezaye kuwafanya imara, sawasawa na Injili yangu na kwa kuhubiriwa kwake Yesu Kristo, sawasawa na ufunuo wa ile siri iliyositirika tangu zamani za milele, 26#2 Tim 1:10; Rum 1:5 ikadhihirishwa wakati huu kwa maandiko ya manabii, ikajulikana na mataifa yote kama alivyoamuru Mungu wa milele, ili waitii Imani. 27#1 Tim 1:17; Yud 1:25 Ndiye Mungu mwenye hekima peke yake. Utukufu una yeye kwa Yesu Kristo, milele na milele. Amina.

Iliyochaguliwa sasa

Warumi 16: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha