Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 92:1-8

Zaburi 92:1-8 SRUV

Ni neno jema kumshukuru BWANA, Na kuliimbia jina lako sifa, Ee Uliye Juu. Kuzitangaza rehema zako asubuhi, Na uaminifu wako wakati wa usiku. Kwa chombo chenye nyuzi kumi, Na kwa kinanda, Na kwa mlio wa kinubi. Kwa kuwa umenifurahisha, BWANA, Kwa kazi yako; nitashangilia Kwa ajili ya matendo ya mikono yako. Ee BWANA, jinsi yalivyo makuu matendo yako! Mawazo yako ni mafumbo makubwa. Mtu mjinga hayatambui hayo, Wala mpumbavu hayafahamu. Hata wasio haki wakichipuka kama majani Na wote watendao maovu wakastawi. Mwishowe wataangamizwa milele; Bali Wewe, BWANA, U Mtukufu hata milele.

Soma Zaburi 92

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha