Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 37

37
Mahimizo ya kuwa na uvumilivu na imani
Ya Daudi.
1Usihangaike kwa sababu ya watenda mabaya,
Usiwahusudu wafanyao ubatili.
2Maana kama majani watakatika mara,
Kama miche mibichi watanyauka.
3Umtumaini BWANA ukatende mema,
Ukae katika nchi, upendezwe na uaminifu.
4 # Ayu 27:10; Wim 2:3; Isa 58:14; 1 Pet 1:8 Nawe ujifurahishe katika BWANA,
Naye atakutimizia haja za moyo wako.
5 # Mt 6:25; 1 Pet 5:7 Umkabidhi BWANA njia yako,
Pia umtumainie, naye atakutendea.
6 # Mik 7:9 Ataitokeza haki yako kama nuru,
Na hukumu yako kama jina la adhuhuri.
7Utulie mbele za BWANA,
Nawe umngojee kwa subira;
Usihangaike juu ya afanikiwaye katika njia yake,
Wala mtu apangaye maovu.
8 # Ayu 5:2; Zab 73:3; Mit 14:29; Efe 4:26; Yak 1:19 Ukomeshe hasira, uache ghadhabu,
Usikasirike, mwisho wake ni kutenda mabaya.
9Maana watenda mabaya watakatiliwa mbali,
Bali wamngojao BWANA ndio watakaoirithi nchi.
10Maana bado kitambo kidogo asiye haki hatakuwapo,
Utapaangalia mahali pake wala hatakuwapo.
11 # Mt 5:5 Bali wenye upole watairithi nchi,
Watajifurahisha kwa wingi wa amani.
12Asiye haki hunuia mabaya juu ya mwenye haki,
Na kumsagia meno yake.
13 # 1 Sam 26:10 BWANA atamcheka,
Maana ameona kwamba siku yake inakuja.
14Wasio haki wamefuta upanga na kupinda uta,
Wamwangushe chini maskini na mhitaji,
Na kuwaua wenye mwenendo wa unyofu.
15Upanga wao utaingia mioyoni mwao wenyewe,
Na nyuta zao zitavunjika.
16 # Mit 15:16; 1 Tim 6:6 Kidogo alicho nacho mwenye haki ni bora
Kuliko wingi wa mali wa wasio haki wengi.
17Maana mikono ya wasio haki itavunjika,
Bali BWANA huwategemeza wenye haki.
18 # Zab 1:6; Isa 60:21 BWANA huwatunza waaminifu,
Na urithi wao utakuwa wa milele.
19 # Ayu 5:20 Hawataaibika wakati wa ubaya,
Na siku za njaa watashiba.
20Bali wasio haki watapotea,
Nao wamchukiao BWANA watatoweka,
Kama uzuri wa mashamba,
Kama moshi watatoweka.
21Asiye haki hukopa wala halipi,
Bali mwenye haki hufadhili, hukirimu.
22 # Mit 3:33 Maana waliobarikiwa na BWANA watairithi nchi,
Nao waliolaaniwa naye watakatiliwa mbali.
23 # Zab 121:3; Mit 16:9 Hatua za mtu mwema huimarishwa na BWANA,
Naye huipenda njia yake.
24 # Mik 7:8; 2 Kor 4:9 Ajapojikwaa hataanguka chini,
Maana BWANA humshika mkono na kumtegemeza.
25Nilikuwa kijana na sasa ni mzee,
Lakini sijamwona mwenye haki ameachwa
Wala mzawa wake akiomba chakula.
26Mchana kutwa hufadhili na kukopesha,
Na mzao wake hubarikiwa.
27Jiepushe na uovu, utende mema,
Na kukaa hata milele.
28 # Zab 11:7 Kwa kuwa BWANA hupenda haki,
Wala hawaachi watauwa wake.
Wao hulindwa milele,
Bali mzawa wa wasio haki ataharibiwa.
29Wenye haki watairithi nchi,
Nao watakaa humo milele.
30Kinywa chake mwenye haki hunena hekima,
Na ulimi wake husema hukumu.
31Sheria ya Mungu wake imo moyoni mwake.
Hatua zake hazitelezi.
32Mtu asiye haki humvizia mwenye haki,
Na kutafuta jinsi ya kumwua.
33 # Zab 109:31 BWANA hatamwacha mkononi mwake,
Wala hatamwacha alaumiwe atakapohukumiwa.
34Wewe umngoje BWANA,
Uishike njia yake,
Naye atakutukuza uirithi nchi,
Utawaona Wasio haki wakiangamizwa.
35Nimemwona mtu asiye haki mkali sana,
Akijieneza kama mwerezi wa Lebanoni.
36Nikapita na kumbe! Hayuko,
Nikamtafuta wala hakuonekana.
37 # Ayu 1:1; Isa 32:17; Lk 2:25-30; Mdo 7:59,60; 1 The 4:17; 2 Tim 4:6-8; 2 Pet 1:14 Umwangalie sana mtu mkamilifu,
Umtazame mtu mnyofu,
Maana mwisho wake mtu huyo ni amani.
38Wakosaji wataangamizwa pamoja,
Wasio haki mwisho wao wataharibiwa.
39 # Zab 3:8; Isa 12:2; Yon 2:8 Na wokovu wa wenye haki una BWANA;
Yeye ni ngome yao wakati wa taabu.
40 # 1 Nya 5:20; Dan 3:17 Naye BWANA huwasaidia na kuwaopoa;
Huwaopoa kutoka kwa wasio haki na kuwaponya;
Kwa kuwa wamemtumaini Yeye.

Iliyochaguliwa sasa

Zaburi 37: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha