Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 21:8-13

Zaburi 21:8-13 SRUV

Mkono wako utawapata adui zako wote, Mkono wako wa kulia utawapata wanaokuchukia. Utawafanya kuwa kama tanuri ya moto, Wakati wa ghadhabu yako. BWANA atawameza kwa ghadhabu yake, Na moto utawateketeza. Matunda yao utayaharibu na kuyaondoa katika nchi, Na wazao wao katika wanadamu. Wakipanga kukutenda mabaya, Kwa miango ya hila, hawatafanikiwa. Kwa maana utawatimua utawafanya wakimbie, Kwa upote wa uta wako utazilenga nyuso zao. Ee BWANA, utukuzwe kwa nguvu zako, Nasi tutaimba na kuuhimidi uwezo wako.

Soma Zaburi 21