Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 21:8-13

Zaburi 21:8-13 NENO

Mkono wako utawashika adui zako wote, mkono wako wa kuume utawakamata adui zako. Wakati utajitokeza, utawafanya kama tanuru la moto. Katika ghadhabu yake BWANA atawameza, moto wake utawateketeza. Utawaangamiza wazao wao kutoka duniani, uzao wao kutoka wanadamu. Ingawa watapanga mabaya dhidi yako na kutunga hila, hawawezi kufanikiwa, kwa kuwa utawafanya wakimbie utakapowalenga usoni pao kwa mshale kutoka upinde wako. Ee BWANA, utukuzwe katika nguvu zako, tutaimba na kusifu nguvu zako.