Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 145:1-9

Zaburi 145:1-9 SRUV

Ee Mungu wangu, Mfalme, nitakutukuza, Nitalihimidi jina lako milele na milele. Kila siku nitakuhimidi, Nitalisifu jina lako milele na milele. BWANA ndiye mkuu mwenye kusifiwa sana, Wala ukuu wake hauchunguziki. Kizazi kwa kizazi kitayasifu matendo yako, Kitayatangaza matendo yako makuu. Nitaifikiri fahari ya utukufu wa adhama yako, Na matendo yako yote ya ajabu. Watu watayataja matendo yako ya kutisha, Nami nitausimulia ukuu wako. Watasimulia juu ya ukuu wa wema wako mwingi. Na wataiimba haki yako kwa sauti. BWANA ni mwenye fadhili na huruma, Si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema, BWANA ni mwema kwa watu wote, Na rehema zake ziko juu ya vyote alivyoumba.

Soma Zaburi 145