Zaburi 145:1-9
Zaburi 145:1-9 NENO
Nitakutukuza wewe, Mungu wangu Mfalme, nitalisifu jina lako milele na milele. Kila siku nitakusifu na kulitukuza jina lako milele na milele. BWANA ni mkuu, anayestahili kusifiwa sana, ukuu wake haupimiki. Kizazi kimoja kitasifia kazi zako kwa kizazi kingine, watasimulia matendo yako makuu. Watasema juu ya utukufu wa fahari ya ukuu wako, nami nitatafakari juu ya kazi zako za ajabu. Watasimulia uwezo wa kazi zako za kutisha, nami nitatangaza matendo yako makuu. Wataadhimisha wema wako mwingi, na wataimba kwa shangwe kuhusu haki yako. BWANA ni mwenye neema na mwingi wa huruma, si mwepesi wa hasira, bali ni mwingi wa upendo. BWANA ni mwema kwa wote, ana huruma kwa vyote alivyovifanya.