Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 127:1-5

Zaburi 127:1-5 SRUV

BWANA asipoijenga nyumba Waijengao wanafanya kazi bure. BWANA asipoulinda mji Yeye aulindaye anakesha bure. Kazi yenu ni bure, mnaoamka mapema, Na kukawia kwenda kulala, Na kula chakula cha taabu; Yeye humpa mpenzi wake usingizi. Tazama, watoto ni urithi kutoka kwa BWANA, Uzao wa tumbo ni thawabu. Kama mishale mkononi mwa shujaa, Ndivyo walivyo watoto wa ujanani. Heri mtu yule Aliyelijaza podo lake hivyo. Naam, hawataona aibu Wanaposema na adui langoni.

Soma Zaburi 127