Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 106:24-35

Zaburi 106:24-35 SRUV

Wakaidharau nchi ile ya kupendeza, Wala hawakuliamini neno lake. Bali wakanung'unika hemani mwao, Wala hawakuisikiliza sauti ya BWANA. Ndipo alipowainulia mkono wake na kuwaapia, Ya kuwa atawaangamiza jangwani, Na kuwatawanya wazao wao kati ya mataifa, Na kuwatapanya katika nchi mbali. Wakamwabudu Baal-Peori, Wakazila dhabihu zilizotolewa kwa wafu. Wakamkasirisha kwa matendo yao; Tauni ikawashambulia. Ndipo Finehasi akasimama akafanya hukumu; Tauni ikazuiliwa. Akahesabiwa kuwa ana haki Kizazi baada ya kizazi hata milele. Wakamghadhabisha penye maji ya Meriba, Hasara ikampata Musa kwa ajili yao, Kwa sababu waliiasi roho yake, Akasema yasiyofaa kwa midomo yake. Hawakuwaangamiza watu wa nchi Kama BWANA alivyowaambia; Bali walijichanganya na mataifa, Wakajifunza matendo yao.

Soma Zaburi 106