Mithali 20:13-15
Mithali 20:13-15 SRUV
Usipende usingizi usije ukawa maskini; Fumbua macho yako nawe utashiba chakula. Haifai kitu, haifai kitu, asema mnunuzi; Lakini akiisha kwenda zake hujisifu. Dhahabu iko, na marijani tele; Lakini midomo ya maarifa ni kito cha thamani.