Methali 20:13-15
Methali 20:13-15 Biblia Habari Njema (BHN)
Usipende kulala tu usije ukawa maskini; uwe macho nawe utakuwa na chakula kingi. “Hakifai, hakifai”, mnunuzi hulalamika, lakini akiondoka hujisifu amepunguziwa bei. Kuna dhahabu na wingi wa mawe ya thamani kubwa; lakini cha thamani kubwa zaidi ni maneno ya busara!
Methali 20:13-15 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Usipende usingizi usije ukawa maskini; Fumbua macho yako nawe utashiba chakula. Haifai kitu, haifai kitu, asema mnunuzi; Lakini akiisha kwenda zake hujisifu. Dhahabu iko, na marijani tele; Lakini midomo ya maarifa ni kito cha thamani.
Methali 20:13-15 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Usipende usingizi usije ukawa maskini; Fumbua macho yako nawe utashiba chakula. Haifai kitu, haifai kitu, asema mnunuzi; Lakini akiisha kwenda zake hujisifu. Dhahabu iko, na marijani tele; Lakini midomo ya maarifa ni kito cha thamani.
Methali 20:13-15 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Usiupende usingizi la sivyo utakuwa maskini, uwe macho nawe utakuwa na chakula cha akiba. “Haifai, haifai!” asema mnunuzi, kisha huondoka akijisifia ununuzi wake. Kuna dhahabu, na marijani kwa wingi, lakini midomo inayonena maarifa ni kito cha thamani.