Mithali 19:10-12
Mithali 19:10-12 SRUV
Maisha ya anasa hayampasi mpumbavu; Sembuse mtumwa awatawale wakuu. Busara ya mtu huiahirisha hasira yake; Nayo ni fahari yake kusamehe makosa. Ghadhabu ya mfalme ni kama ngurumo ya simba; Bali hisani yake kama umande juu ya majani.