Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ayubu 36:26-33

Ayubu 36:26-33 SRUV

Tazama, Mungu ni mkuu, nasi hatumjui; Hesabu ya miaka yake haichunguziki. Maana yeye huvuta juu matone ya maji, Yamwagikayo katika mvua kutoka ukungu wake; Ambayo mawingu yainyesha Na kudondoza juu ya wanadamu kwa wingi. Naam, mtu aweza kuelewa matandazo ya mawingu, Ngurumo za makao yake? Tazama, yeye huutandaza mwanga wake, umzunguke; Naye hufunika vilindi vya bahari. Kwani huwahukumu makabila ya watu kwa njia hizi; Hutoa chakula kwa ukarimu. Yeye huifunika mikono yake kwa umeme; Na kuuagiza shabaha utakayopiga. Mshindo wake hutoa habari zake, Anayewaka hasira juu ya uovu.

Soma Ayubu 36