Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yobu 36:26-33

Yobu 36:26-33 BHN

Mungu ni mkuu mno hata hatuwezi kumjua; muda wa maisha yake hauchunguziki. Yeye huyavuta kwake maji ya bahari, na kutoka ukungu hufanya matone ya mvua. Huyafanya mawingu yanyeshe mvua, na kuwatiririshia binadamu kwa wingi. Nani ajuaye jinsi mawingu yatandavyo, au jinsi radi ingurumavyo angani kwake? Yeye huutandaza umeme wake kumzunguka, na kuvifunika vilindi vya bahari. Kwa mvua huwalisha watu na kuwapatia chakula kwa wingi. Huukamata umeme kwa mikono yake, kisha hulenga nao shabaha, Radi hutangaza ujio wake Mungu, hata wanyama hujua kwamba anakuja.

Soma Yobu 36