Isaya 51:15-16
Isaya 51:15-16 SRUV
Maana mimi ni BWANA, Mungu wako, niichafuaye bahari, mawimbi yake yakavuma. BWANA wa majeshi ndilo jina lake. Nami nimetia maneno yangu kinywani mwako, nami nimekusitiri katika kivuli cha mkono wangu, ili nizipande mbingu, na kuiweka misingi ya dunia, na kuuambia Sayuni, Ninyi ni watu wangu.