Isaya 51:15-16
Isaya 51:15-16 Biblia Habari Njema (BHN)
Mimi ni Mwenyezi-Mungu, Mungu wako; nivurugaye bahari, mawimbi yake yakanguruma; Mwenyezi-Mungu wa majeshi, ndilo jina langu! Nimeyaweka maneno yangu mdomoni mwako; nimekuficha katika kivuli cha mkono wangu. Mimi nilizitandaza mbingu, nikaiweka misingi ya dunia. Mimi nawaambieni enyi watu wa Siyoni: ‘Nyinyi ni watu wangu.’”
Isaya 51:15-16 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Maana mimi ni BWANA, Mungu wako, niichafuaye bahari, mawimbi yake yakavuma. BWANA wa majeshi ndilo jina lake. Nami nimetia maneno yangu kinywani mwako, nami nimekusitiri katika kivuli cha mkono wangu, ili nizipande mbingu, na kuiweka misingi ya dunia, na kuuambia Sayuni, Ninyi ni watu wangu.
Isaya 51:15-16 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Maana mimi ni BWANA, Mungu wako, niichafuaye bahari, mawimbi yake yakavuma. BWANA wa majeshi ndilo jina lake. Nami nimetia maneno yangu kinywani mwako, nami nimekusitiri katika kivuli cha mkono wangu, ili nizipande mbingu, na kuiweka misingi ya dunia, na kuuambia Sayuni, Ninyi ni watu wangu.
Isaya 51:15-16 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Kwa maana Mimi ndimi BWANA, Mungu wako, ambaye huisukasuka bahari ili mawimbi yake yangurume: BWANA wa majeshi ndilo jina lake. Nimeweka maneno yangu kinywani mwako na kukufunika kwa uvuli wa mkono wangu: Mimi niliyeweka mbingu mahali pake, niliyeweka misingi ya dunia, niwaambiaye Sayuni, ‘Ninyi ni watu wangu.’ ”