Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mwanzo 24:52-53

Mwanzo 24:52-53 NENO

Ikawa huyo mtumishi wa Abrahamu aliposikia waliyosema, alisujudu, uso wake ukagusa chini mbele za BWANA. Ndipo huyo mtumishi akatoa vitu vilivyotengenezwa kwa dhahabu na kwa fedha, pamoja na mavazi, akampa Rebeka; pia akawapa zawadi za thamani kubwa nduguye na mamaye.