Wim 7:11-12
Wim 7:11-12 SUV
Njoo, mpendwa wangu, twende mashambani, Tufanye maskani katika vijiji. Twende mapema hata mashamba ya mizabibu, Tuone kama mzabihu umechanua, Na maua yake yamefunuka; Kama mikomamanga imetoa maua; Huko nitakupa pambaja zangu.