Wim 6:1-3
Wim 6:1-3 SUV
Mpendwa wako amekwenda wapi, Wewe uliye mzuri katika wanawake? Mpendwa wako amegeukia upande upi, Ili tumtafute pamoja nawe? Mpendwa wangu ameshukia bustani yake, Kwenye matuta ya rihani; Ili kulisha penye bustani, Ili kuchuma nyinyoro. Mimi ni wake mpendwa wangu, naye ni wangu, Hulisha kundi lake penye nyinyoro.