Wimbo Ulio Bora 6:1-3
Wimbo Ulio Bora 6:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Ewe mwanamke uliye mzuri sana; amekwenda wapi huyo mpenzi wako? Ameelekea wapi mpenzi wako ili tupate kushirikiana nawe katika kumtafuta? Mpenzi wangu amekwenda bustanini mwake, mahali ambapo rihani hustawi. Yeye analisha kondoo wake na kukusanya yungiyungi. Mimi ni wake mpenzi wangu, naye ni wangu; yeye huwalisha kondoo wake penye yungiyungi.
Wimbo Ulio Bora 6:1-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mpendwa wako amekwenda wapi, Wewe uliye mzuri katika wanawake? Mpendwa wako amegeukia upande upi, Ili tumtafute pamoja nawe? Mpendwa wangu ameshukia bustani yake, Kwenye matuta ya rihani; Ili kulisha penye bustani, Ili kuchuma nyinyoro. Mimi ni wake mpendwa wangu, naye ni wangu, Hulisha kundi lake penye nyinyoro.
Wimbo Ulio Bora 6:1-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mpendwa wako amekwenda wapi, Wewe uliye mzuri katika wanawake? Mpendwa wako amegeukia upande upi, Ili tumtafute pamoja nawe? Mpendwa wangu ameshukia bustani yake, Kwenye matuta ya rihani; Ili kulisha penye bustani, Ili kuchuma nyinyoro. Mimi ni wake mpendwa wangu, naye ni wangu, Hulisha kundi lake penye nyinyoro.
Wimbo Ulio Bora 6:1-3 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Mpenzi wako ameenda wapi, ewe mzuri kupita wanawake wote? Mpenzi wako amegeukia njia ipi, tupate kumtafuta pamoja nawe? Mpenzi wangu ameenda bustanini mwake, kwenye vitalu vya vikolezo, kujilisha bustanini na kukusanya yungiyungi. Mimi ni wake mpenzi wangu, na mpenzi wangu ni wangu; yeye hujilisha kati ya yungiyungi.