Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Rum 14

14
Usimhukumu Mwingine
1 # Kol 2:16; Rum 15:1; 1 Kor 8:9 Yeye aliye dhaifu wa imani, mkaribisheni, walakini msimhukumu mawazo yake. 2#Mwa 1:29; 9:3Mtu mmoja anayo imani, anakula vyote; lakini yeye aliye dhaifu hula mboga. 3#Kol 2:16Yeye alaye asimdharau huyo asiyekula, wala yeye asiyekula asimhukumu huyo alaye; kwa maana Mungu amemkubali. 4#Mt 7:1; Yak 4:11,12Wewe u nani unayemhukumu mtumishi wa mwingine? Kwa bwana wake mwenyewe yeye husimama au huanguka. Naam, atasimamishwa, kwa kuwa Bwana aweza kumsimamisha. 5#Gal 4:10Mtu mmoja afanya tofauti kati ya siku na siku, mwingine aona siku zote kuwa sawasawa. Kila mtu na athibitike katika akili zake mwenyewe. 6Yeye aadhimishaye siku, huiadhimisha kwa Bwana; naye alaye, hula kwa Bwana, kwa maana amshukuru Mungu; tena asiyekula, hali kwa Bwana, naye pia amshukuru Mungu. 7Kwa sababu hakuna mtu miongoni mwetu aishiye kwa nafsi yake, wala hakuna afaye kwa nafsi yake. 8#Gal 2:20; 1 The 5:10; Lk 20:38Kwa maana kama tukiishi, twaishi kwa Bwana, au kama tukifa, twafa kwa Bwana. Basi kama tukiishi au kama tukifa, tu mali ya Bwana. 9Maana Kristo alikufa akawa hai tena kwa sababu hii, awamiliki waliokufa na walio hai pia.
10 # 2 Kor 5:10; Mdo 17:31; Mt 25:31,32 Lakini wewe je! Mbona wamhukumu ndugu yako? Au wewe je! Mbona wamdharau ndugu yako? Kwa maana sisi sote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Mungu. 11#Isa 45:23; 49:18; Flp 2:10,11Kwa kuwa imeandikwa,
Kama niishivyo, anena Bwana, kila goti litapigwa mbele zangu;
Na kila ulimi utamkiri Mungu.
12 # Gal 6:5 Basi ni hivyo, kila mtu miongoni mwetu atatoa habari zake mwenyewe mbele za Mungu.
Usimkwaze Mwingine
13Basi tusizidi kuhukumiana, bali afadhali toeni hukumu hii, mtu asitie kitu cha kumkwaza ndugu au cha kumwangusha. 14#Mt 15:11; Mdo 10:15; Tit 1:15Najua, tena nimehakikishwa sana katika Bwana Yesu, ya kuwa hakuna kitu kilicho najisi kwa asili yake, lakini kwake yeye akionaye kitu kuwa najisi, kwake huyo kitu kile ni najisi. 15#1 Kor 8:11-13Na ndugu yako akiingia huzuni kwa sababu ya chakula, umeacha kwenda katika upendo. Kwa chakula chako usimharibu mtu yule ambaye Kristo alikufa kwa ajili yake. 16#Tit 2:5Basi, huo wema wenu usitajwe kwa ubaya. 17#Lk 17:20Maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu. 18Kwa kuwa yeye amtumikiaye Kristo katika mambo hayo humpendeza Mungu, tena hukubaliwa na wanadamu. 19#Rum 12:18; 15:2Basi kama ni hivyo, na mfuate mambo ya amani na mambo yafaayo kwa kujengana. 20Kwa ajili ya chakula usiiharibu kazi ya Mungu. Kweli, vyote ni safi; bali ni vibaya kwa mtu alaye na kujikwaza. 21#1 Kor 8:13Ni vyema kutokula nyama wala kunywa divai wala kutenda neno lo lote ambalo kwa hilo ndugu yako hukwazwa. 22Ile imani uliyo nayo uwe nayo nafsini mwako mbele za Mungu. Heri mtu yule asiyejihukumu nafsi yake katika neno lile analolikubali. 23#Tit 1:15Lakini aliye na shaka, kama akila, amehukumiwa kuwa ana hatia, kwa maana hakula kwa imani. Na kila tendo lisilotoka katika imani ni dhambi.

Iliyochaguliwa sasa

Rum 14: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha