Zab 98:7-9
Zab 98:7-9 SUV
Bahari na ivume na vyote viijazavyo, Ulimwengu nao wanaokaa ndani yake. Mito na ipige makofi, Milima na iimbe pamoja kwa furaha. Mbele za BWANA; Kwa maana anakuja aihukumu nchi. Atauhukumu ulimwengu kwa haki, Na mataifa kwa adili.