Zaburi 98:7-9
Zaburi 98:7-9 Biblia Habari Njema (BHN)
Bahari na ivume na vyote vilivyomo; dunia na wote waishio ndani yake. Enyi mito pigeni makofi; enyi vilima imbeni pamoja kwa shangwe. Shangilieni mbele ya Mwenyezi-Mungu, maana anakuja kutawala dunia. Atauhukumu ulimwengu kwa haki, atawatawala watu kwa uadilifu.
Zaburi 98:7-9 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Bahari na ivume na vyote viijazavyo, Ulimwengu nao wanaokaa ndani yake. Mito na ipige makofi, Milima na iimbe pamoja kwa furaha. Mbele za BWANA; Kwa maana anakuja kuihukumu nchi. Atauhukumu ulimwengu kwa uaminifu, Na mataifa kwa adili.
Zaburi 98:7-9 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Bahari na ivume na vyote viijazavyo, Ulimwengu nao wanaokaa ndani yake. Mito na ipige makofi, Milima na iimbe pamoja kwa furaha. Mbele za BWANA; Kwa maana anakuja aihukumu nchi. Atauhukumu ulimwengu kwa haki, Na mataifa kwa adili.
Zaburi 98:7-9 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Bahari na ivume na kila kilicho ndani yake, dunia na wote wanaoishi ndani yake. Mito na ipige makofi, milima na iimbe pamoja kwa furaha, vyote na viimbe mbele za BWANA, kwa maana yuaja kuhukumu dunia. Atahukumu dunia kwa haki na mataifa kwa haki.