BWANA, watesi wangu wamezidi kuwa wengi, Ni wengi wanaonishambulia, Ni wengi wanaoiambia nafsi yangu, Hana wokovu huyu kwa Mungu. Na Wewe, BWANA, U ngao yangu pande zote, Utukufu wangu na mwinua kichwa changu. Kwa sauti yangu namwita BWANA Naye aniitikia toka mlima wake mtakatifu. Nalijilaza nikalala usingizi, nikaamka, Kwa kuwa BWANA ananitegemeza. Sitayaogopa makumi elfu ya watu, Waliojipanga juu yangu pande zote. BWANA, uinuke, Mungu wangu, uniokoe, Maana umewapiga taya adui zangu wote; Umewavunja meno wasio haki. Wokovu una BWANA; Baraka yako na iwe juu ya watu wako.
Soma Zab 3
Shirikisha
Linganisha Matoleo Yote: Zab 3:1-8
Hifadhi mistari, soma bila mtandao, tazama klipu za mafunzo, na zaidi!
YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video