Zab 3:1-4
Zab 3:1-4 SUV
BWANA, watesi wangu wamezidi kuwa wengi, Ni wengi wanaonishambulia, Ni wengi wanaoiambia nafsi yangu, Hana wokovu huyu kwa Mungu. Na Wewe, BWANA, U ngao yangu pande zote, Utukufu wangu na mwinua kichwa changu. Kwa sauti yangu namwita BWANA Naye aniitikia toka mlima wake mtakatifu.