Zab 22:16-19
Zab 22:16-19 SUV
Kwa maana mbwa wamenizunguka; Kusanyiko la waovu wamenisonga; Wamenizua mikono na miguu. Naweza kuihesabu mifupa yangu yote; Wao wananitazama na kunikodolea macho. Wanagawanya nguo zangu, Na vazi langu wanalipigia kura. Nawe, BWANA, usiwe mbali, Ee Nguvu zangu, fanya haraka kunisaidia.