Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 22

22
Ombi la Ukombozi katika Shida na Ukatili
Kwa mwimbishaji: kwa kufuata mtindo wa utenzi wa Kulungu wa Alfajiri. Zaburi ya Daudi.
1 # Mt 27:46; Mk 15:34; Ebr 5:7 Mungu wangu, Mungu wangu,
Mbona umeniacha?
Mbona U mbali na wokovu wangu,
Na maneno ya kuugua kwangu?
2Ee Mungu wangu, nalia mchana lakini hujibu
Na wakati wa usiku lakini sipati raha.
3 # Isa 6:3; Ufu 4:8 Na Wewe U Mtakatifu,
Uketiye juu ya sifa za Israeli.
4Baba zetu walikutumaini Wewe,
Walitumaini, na Wewe ukawaokoa.
5Walikulilia Wewe wakaokoka,
Walikutumaini wasiaibike.
6 # Isa 53:3 Lakini mimi ni mdudu wala si mtu,
Laumu ya wanadamu na mzaha wa watu.
7 # Mt 27:39; 9:24; Mk 15:20,29; Lk 23:35; 16:14 Wote wanionao hunicheka sana,
Hunifyonya, wakitikisa vichwa vyao;
8 # Mt 27:43 Husema, Umtegemee BWANA; na amponye;
Na amwokoe sasa, maana apendezwa naye.
9Naam, Wewe ndiwe uliyenitoa tumboni,
Ulinitumainisha matitini mwa mama yangu.
10Kwako nalitupwa tangu tumboni,
Toka tumboni mwa mamangu ndiwe Mungu wangu.
11Usiwe mbali nami maana taabu i karibu,
Kwa maana hakuna msaidizi.
12Mafahali wengi wamenizunguka,
Walio hodari wa Bashani wamenisonga;
13 # Zab 35:21; 1 Pet 5:8 Wananifumbulia vinywa vyao,
Kama simba apapuraye na kunguruma.
14Nimemwagika kama maji,
Mifupa yangu yote imeteguka,
Moyo wangu umekuwa kama nta,
Na kuyeyuka ndani ya mtima wangu.
15 # Mit 17:22 Nguvu zangu zimekauka kama gae,
Ulimi wangu waambatana na taya zangu;
Unaniweka katika mavumbi ya mauti
16 # Zek 12:10; Lk 23:33; Yn 20:27 Kwa maana mbwa wamenizunguka;
Kusanyiko la waovu wamenisonga;
Wamenizua mikono na miguu.
17Naweza kuihesabu mifupa yangu yote;
Wao wananitazama na kunikodolea macho.
18 # Mt 27:35; Mk 15:24; Lk 23:34; Yn 19:24 Wanagawanya nguo zangu,
Na vazi langu wanalipigia kura.
19Nawe, BWANA, usiwe mbali,
Ee Nguvu zangu, fanya haraka kunisaidia.
20Uniponye nafsi yangu na upanga,
Mpenzi wangu na nguvu za mbwa.
21 # 2 Tim 4:17 Kinywani mwa simba uniokoe;
Naam, toka pembe za nyati umenijibu.
22 # Ebr 2:12; Yn 20:17 Nitalihubiri jina lako kwa ndugu zangu,
Katikati ya kusanyiko nitakusifu.
23Ninyi mnaomcha BWANA, msifuni,
Enyi nyote mlio wazao wa Yakobo, mtukuzeni,
Mcheni, enyi nyote mlio wazao wa Israeli.
24Maana hakulidharau teso la mteswa,
Wala hakuchukizwa nalo;
Wala hakumficha uso wake,
Bali alipomlilia akamsikia.
25Kwako zinatoka sifa zangu
Katika kusanyiko kubwa.
Nitaziondoa nadhiri zangu
Mbele yao wamchao.
26 # Yn 6:51,57 Wapole watakula na kushiba,
Wamtafutao BWANA watamsifu;
Mioyo yenu na iishi milele.
27 # Zab 2:8 Miisho yote ya dunia itakumbuka,
Na watu watamrejea BWANA;
Jamaa zote za mataifa watamsujudia.
28 # Zab 47:7-9; Zek 14:9; Mt 6:13 Maana ufalme una BWANA,
Naye ndiye awatawalaye mataifa.
29 # Isa 26:19 Wakwasi wote wa dunia watakula na kusujudu,
Humwinamia wote washukao mavumbini;
Naam, yeye asiyeweza kujihuisha nafsi yake,
30Wazao wake watamtumikia.
Zitasimuliwa habari za BWANA,
Kwa kizazi kitakachokuja,
31Nao watawahubiri watakaozaliwa haki yake,
Ya kwamba ndiye aliyeyafanya.

Iliyochaguliwa sasa

Zab 22: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha