Zab 143:4-7
Zab 143:4-7 SUV
Na roho yangu imezimia ndani yangu, Moyo wangu ndani yangu umesituka. Nimezikumbuka siku za kale, Nimeyatafakari matendo yako yote, Naziwaza kazi za mikono yako. Nakunyoshea mikono yangu; Nafsi yangu inakuonea kiu kama nchi kame. Ee BWANA, unijibu hima, roho yangu imelegea; Usinifiche uso wako, Nisifanane nao washukao shimoni