Zaburi 143:4-7
Zaburi 143:4-7 Biblia Habari Njema (BHN)
Nimevunjika moyo kabisa; nimekufa ganzi kwa ajili ya woga. Nakumbuka siku zilizopita; natafakari juu ya yote uliyotenda, nawaza na kuwazua juu ya matendo yako. Nakunyoshea mikono yangu kuomba; nina kiu yako kama nchi kavu isiyo na maji. Ee Mwenyezi-Mungu, unijibu haraka; maana nimekata tamaa kabisa! Usijifiche mbali nami, nisije nikawa kama wale washukao kwa wafu.
Zaburi 143:4-7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Na roho yangu imezimia ndani yangu, Moyo wangu ndani yangu umeshtuka. Nimezikumbuka siku za kale, Nimeyatafakari matendo yako yote, Naziwaza kazi za mikono yako. Nakunyoshea mikono yangu; Nafsi yangu inakuonea kiu kama nchi kame. Ee BWANA, unijibu hima, roho yangu imelegea; Usinifiche uso wako, Nisifanane nao washukao shimoni.
Zaburi 143:4-7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Na roho yangu imezimia ndani yangu, Moyo wangu ndani yangu umesituka. Nimezikumbuka siku za kale, Nimeyatafakari matendo yako yote, Naziwaza kazi za mikono yako. Nakunyoshea mikono yangu; Nafsi yangu inakuonea kiu kama nchi kame. Ee BWANA, unijibu hima, roho yangu imelegea; Usinifiche uso wako, Nisifanane nao washukao shimoni
Zaburi 143:4-7 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Kwa hiyo roho yangu inazimia ndani yangu, moyo wangu ndani yangu unakata tamaa. Nakumbuka siku za zamani; natafakari juu ya kazi zako zote, naangalia juu ya kazi ambazo mikono yako imezifanya. Nanyoosha mikono yangu kwako, nafsi yangu inakuonea kiu kama ardhi kame. Ee BWANA, unijibu haraka, roho yangu inazimia. Usinifiche uso wako, ama sivyo nitafanana na wale wanaoshuka shimoni.