Zab 125:1-3
Zab 125:1-3 SUV
Wamtumainio BWANA ni kama mlima Sayuni, Ambao hautatikisika, wakaa milele. Kama milima inavyouzunguka Yerusalemu, Ndivyo BWANA anavyowazunguka watu wake, Tangu sasa na hata milele. Kwa maana fimbo ya udhalimu Haitakaa juu ya fungu la wenye haki; Wenye haki wasije wakainyosha Mikono yao kwenye upotovu.