Zaburi 125:1-3
Zaburi 125:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Wanaomtegemea Mwenyezi-Mungu, wako kama mlima Siyoni, ambao hautikisiki bali wabaki imara daima. Kama Yerusalemu inavyozungukwa na milima, ndivyo Mwenyezi-Mungu awazungukavyo watu wake, tangu sasa na hata milele. Waovu hawataendelea kutawala nchi ya waadilifu; wasije waadilifu nao wakafanya maovu.
Zaburi 125:1-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Wamtumainio BWANA ni kama mlima Sayuni, Ambao hautikisiki, wakaa milele. Kama milima inavyouzunguka Yerusalemu, Ndivyo BWANA anavyowazunguka watu wake, Tangu sasa na hata milele. Kwa maana fimbo ya udhalimu Haitakaa juu ya nchi ya wenye haki; Ili wenye haki wasije wakainyosha Mikono yao kwenye upotovu.
Zaburi 125:1-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Wamtumainio BWANA ni kama mlima Sayuni, Ambao hautatikisika, wakaa milele. Kama milima inavyouzunguka Yerusalemu, Ndivyo BWANA anavyowazunguka watu wake, Tangu sasa na hata milele. Kwa maana fimbo ya udhalimu Haitakaa juu ya fungu la wenye haki; Wenye haki wasije wakainyosha Mikono yao kwenye upotovu.
Zaburi 125:1-3 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Wale wamtumainio BWANA ni kama Mlima Sayuni, ambao hauwezi kutikisika, bali wadumu milele. Kama milima inavyozunguka Yerusalemu, ndivyo BWANA anavyowazunguka watu wake sasa na hata milele. Fimbo ya waovu haitadumu juu ya nchi waliyopewa wenye haki, ili wenye haki wasije wakatumia mikono yao kutenda ubaya.