Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 118:19-29

Zab 118:19-29 SUV

Nifungulieni malango ya haki, Nitaingia na kumshukuru BWANA. Lango hili ni la BWANA, Wenye haki ndio watakaoliingia. Nitakushukuru kwa maana umenijibu, Nawe umekuwa wokovu wangu. Jiwe walilolikataa waashi Limekuwa jiwe kuu la pembeni. Neno hili limetoka kwa BWANA, Nalo ni ajabu machoni petu. Siku hii ndiyo aliyoifanya BWANA, Tutashangilia na kuifurahia. Ee BWANA, utuokoe, twakusihi; Ee BWANA, utufanikishe, twakusihi. Na abarikiwe yeye ajaye kwa jina la BWANA; Tumewabarikia toka nyumbani mwa BWANA. BWANA ndiye aliye Mungu, Naye ndiye aliyetupa nuru. Ifungeni dhabihu kwa kamba Pembeni mwa madhabahu. Ndiwe Mungu wangu, nami nitakushukuru, Ndiwe Mungu wangu, nami nitakutukuza. Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema, Kwa maana fadhili zake ni za milele.

Soma Zab 118

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha