Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 118

118
Wimbo wa Ushindi
1 # 1 Nya 16:18,34; 2 Nya 5:13; 7:3; Ezr 3:11; Zab 100:5; 106:1; 107:1; 136:1; Yer 33:11 Haleluya.
Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema,
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
2 # Zab 115:9 Israeli na aseme sasa,
Ya kwamba fadhili zake ni za milele.
3Mlango wa Haruni na waseme sasa,
Ya kwamba fadhili zake ni za milele.
4Wamchao BWANA na waseme sasa,
Ya kwamba fadhili zake ni za milele.
5 # Zab 18:19 Katika shida yangu nalimwita BWANA;
BWANA akanijibu akaniweka panapo nafasi.
6 # Ebr 13:6 BWANA yuko upande wangu, sitaogopa;
Mwanadamu atanitenda nini?
7 # Zab 54:4 BWANA yuko upande wangu, msaidizi wangu,
Kwa hiyo nitawaona wanaonichukia wameshindwa.
8 # Zab 62:8; Isa 2:22; Yer 17:5,7 Ni heri kumkimbilia BWANA
Kuliko kuwatumainia wanadamu.
9 # Zab 146:3; Isa 30:2,3 Ni heri kumkimbilia BWANA.
Kuliko kuwatumainia wakuu.
10Mataifa yote walinizunguka;
Kwa jina la BWANA naliwakatilia mbali.
11 # Zab 88:17 Walinizunguka, naam, walinizunguka;
Kwa jina la BWANA naliwakatilia mbali.
12 # Kum 1:44; Mhu 7:6 Walinizunguka kama nyuki,
Walizimika kama moto wa miibani;
Kwa jina la BWANA naliwakatilia mbali.
13Ulinisukuma sana ili nianguke;
Lakini BWANA akanisaidia.
14 # Kut 15:2; Isa 12:2 BWANA ni nguvu zangu na wimbo wangu,
Naye amekuwa wokovu wangu.
15Sauti ya furaha na wokovu
Imo hemani mwao wenye haki;
Mkono wa kuume wa BWANA hutenda makuu.
16 # Kut 15:6 Mkono wa kuume wa BWANA umetukuzwa;
Mkono wa kuume wa BWANA hutenda makuu.
17 # Zab 6:5; 73:28 Sitakufa bali nitaishi,
Nami nitayasimulia matendo ya BWANA.
18 # Mit 3:11,12; 1 Kor 11:32 BWANA ameniadhibu sana,
Lakini hakuniacha nife.
19 # Isa 26:2 Nifungulieni malango ya haki,
Nitaingia na kumshukuru BWANA.
20 # Zab 24:7; Isa 35:8 Lango hili ni la BWANA,
Wenye haki ndio watakaoliingia.
21Nitakushukuru kwa maana umenijibu,
Nawe umekuwa wokovu wangu.
22 # Mt 21:42; Mk 12:10; Lk 20:17; Mdo 4:11; Efe 2:20; 1 Pet 2:4,7 # Mt 21:42; Mk 12:10-11 Jiwe walilolikataa waashi
Limekuwa jiwe kuu la pembeni.
23 # Ayu 5:9 Neno hili limetoka kwa BWANA,
Nalo ni ajabu machoni petu.
24 # 2 Kor 6:2 Siku hii ndiyo aliyoifanya BWANA,
Tutashangilia na kuifurahia.
25 # Mt 21:9; Mk 11:9; Yn 12:13 Ee BWANA, utuokoe, twakusihi;
Ee BWANA, utufanikishe, twakusihi.
26 # Zek 4:7; Mt 21:9; 23:39; Mk 11:9; Lk 13:35; 19:38; Yn 12:13 Na abarikiwe yeye ajaye kwa jina la BWANA;
Tumewabarikia toka nyumbani mwa BWANA.
27 # Est 8:16; Mik 7:9; Mal 4:2 BWANA ndiye aliye Mungu,
Naye ndiye aliyetupa nuru.
Ifungeni dhabihu kwa kamba
Pembeni mwa madhabahu.
28 # Kut 15:2; Isa 25:1 Ndiwe Mungu wangu, nami nitakushukuru,
Ndiwe Mungu wangu, nami nitakutukuza.
29Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema,
Kwa maana fadhili zake ni za milele.

Iliyochaguliwa sasa

Zab 118: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha