Mit 9:7-12
Mit 9:7-12 SUV
Amkemeaye mwenye dharau hujipatia fedheha; Amkaripiaye mtu mbaya hujipatia aibu. Usimkaripie mwenye dharau, asije akakuchukia; Mkaripie mwenye hekima, naye atakupenda. Mwelimishe mwenye hekima, naye atazidi kuwa na hekima; Mfundishe mwenye haki, naye atazidi kuwa na elimu; Kumcha BWANA ni mwanzo wa hekima; Na kumjua Mtakatifu ni ufahamu. Maana, kwa msaada wangu siku zako zitazidishwa; Na miaka ya maisha yako itaongezwa. Kama una hekima, una hekima kwa nafsi yako; Na kama una dharau, utaichukua peke yako.