Methali 9:7-12
Methali 9:7-12 Biblia Habari Njema (BHN)
Anayemkosoa mwenye dharau hupata matusi, amkaripiaye mwovu huishia kwa kuumizwa. Usimwonye mwenye dharau maana atakuchukia; mwonye mwenye hekima naye atakupenda. Mfunze mwenye hekima naye atazidi kuwa na hekima; mfundishe mwadilifu naye atazidi kuelimika. Kumcha Mwenyezi-Mungu ni msingi wa hekima; na kumjua yule Mtakatifu ni kupata akili. Kwa msaada wangu mimi Hekima siku zako zitaongezwa; utaongezewa miaka mingi maishani mwako. Kama una hekima, itakufaa wewe mwenyewe; kama ukiidharau, mwenyewe utapata hasara.
Methali 9:7-12 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Amkemeaye mwenye dharau hujipatia fedheha; Amkaripiaye mtu mbaya hujipatia aibu. Usimkaripie mwenye dharau, asije akakuchukia; Mkaripie mwenye hekima, naye atakupenda. Mwelimishe mwenye hekima, naye atazidi kuwa na hekima; Mfundishe mwenye haki, naye atazidi kuwa na elimu; Kumcha BWANA ni mwanzo wa hekima; Na kumjua Mtakatifu ni ufahamu. Maana, kwa msaada wangu siku zako zitazidishwa; Na miaka ya maisha yako itaongezwa. Kama una hekima, una hekima kwa nafsi yako; Na kama una dharau, utaichukua peke yako.
Methali 9:7-12 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Amkemeaye mwenye dharau hujipatia fedheha; Amkaripiaye mtu mbaya hujipatia aibu. Usimkaripie mwenye dharau, asije akakuchukia; Mkaripie mwenye hekima, naye atakupenda. Mwelimishe mwenye hekima, naye atazidi kuwa na hekima; Mfundishe mwenye haki, naye atazidi kuwa na elimu; Kumcha BWANA ni mwanzo wa hekima; Na kumjua Mtakatifu ni ufahamu. Maana, kwa msaada wangu siku zako zitazidishwa; Na miaka ya maisha yako itaongezwa. Kama una hekima, una hekima kwa nafsi yako; Na kama una dharau, utaichukua peke yako.
Methali 9:7-12 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
“Yeyote anayemkosoa mwenye dhihaka hukaribisha matusi; yeyote anayekemea mtu mwovu hupatwa na matusi. Usimkemee mwenye dhihaka, la sivyo atakuchukia; mkemee mwenye hekima naye atakupenda. Mfundishe mtu mwenye hekima naye atakuwa na hekima zaidi; mfundishe mtu mwadilifu naye atazidi kufundishika. “Kumcha BWANA ndicho chanzo cha hekima, na kumjua Aliye Mtakatifu ni ufahamu. Kwa maana kwa msaada wangu siku zako zitakuwa nyingi, na miaka itaongezwa katika maisha yako. Kama wewe una hekima, hekima yako itakupa tuzo; kama wewe ni mtu wa mzaha, wewe mwenyewe ndiwe utateseka.”