Mit 9:10-12
Mit 9:10-12 SUV
Kumcha BWANA ni mwanzo wa hekima; Na kumjua Mtakatifu ni ufahamu. Maana, kwa msaada wangu siku zako zitazidishwa; Na miaka ya maisha yako itaongezwa. Kama una hekima, una hekima kwa nafsi yako; Na kama una dharau, utaichukua peke yako.