Methali 9:10-12
Methali 9:10-12 Biblia Habari Njema (BHN)
Kumcha Mwenyezi-Mungu ni msingi wa hekima; na kumjua yule Mtakatifu ni kupata akili. Kwa msaada wangu mimi Hekima siku zako zitaongezwa; utaongezewa miaka mingi maishani mwako. Kama una hekima, itakufaa wewe mwenyewe; kama ukiidharau, mwenyewe utapata hasara.
Methali 9:10-12 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kumcha BWANA ni mwanzo wa hekima; Na kumjua Mtakatifu ni ufahamu. Maana, kwa msaada wangu siku zako zitazidishwa; Na miaka ya maisha yako itaongezwa. Kama una hekima, una hekima kwa nafsi yako; Na kama una dharau, utaichukua peke yako.
Methali 9:10-12 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kumcha BWANA ni mwanzo wa hekima; Na kumjua Mtakatifu ni ufahamu. Maana, kwa msaada wangu siku zako zitazidishwa; Na miaka ya maisha yako itaongezwa. Kama una hekima, una hekima kwa nafsi yako; Na kama una dharau, utaichukua peke yako.
Methali 9:10-12 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
“Kumcha BWANA ndicho chanzo cha hekima, na kumjua Aliye Mtakatifu ni ufahamu. Kwa maana kwa msaada wangu siku zako zitakuwa nyingi, na miaka itaongezwa katika maisha yako. Kama wewe una hekima, hekima yako itakupa tuzo; kama wewe ni mtu wa mzaha, wewe mwenyewe ndiwe utateseka.”