Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mit 3:21-26

Mit 3:21-26 SUV

Mwanangu, yasiondoke haya machoni pako, Shika hekima kamili na busara. Basi yatakuwa uzima kwa nafsi yako, Na neema shingoni mwako. Ndipo utakapokwenda katika njia yako salama, Wala mguu wako hautakwaa. Ulalapo hutaona hofu; Naam, utalala na usingizi wako utakuwa mtamu. Usiogope hofu ya ghafula, Wala uharibifu wa waovu utakapofika. Kwa kuwa BWANA atakuwa tumaini lako, Naye atakulinda mguu wako usinaswe.

Soma Mit 3