Mit 27:15-27
Mit 27:15-27 SUV
Kutona-tona daima siku ya mvua nyingi, Na mwanamke mgomvi ni sawasawa; Atakaye kumzuia huyo huuzuia upepo; Na mkono wake wa kuume hukuta mafuta. Chuma hunoa chuma; Ndivyo mtu aunoavyo uso wa rafiki yake. Yeye autunzaye mtini atakula matunda yake; Naye amhudumiaye bwana wake ataheshimiwa. Kama uso ufananavyo na uso katika maji; Kadhalika moyo wa mtu na mwenzake. Kuzimu na Uharibifu havishibi; Wala macho ya wanadamu hayashibi. Kalibu ni kwa fedha, na tanuru kwa dhahabu; Na mtu hujaribiwa kwa sifa zake. Hata ukimtwanga mpumbavu kwa mchi kinuni pamoja na ngano; Upumbavu wake hautamtoka. Fanya bidii kuijua hali ya makundi yako; Na kuwaangalia sana ng’ombe zako. Kwa maana mali haziwi za milele; Na taji je! Yadumu tangu kizazi hata kizazi? Manyasi huchukuliwa, na majani mabichi huonekana, Na maboga ya milimani hukusanyika. Wana-kondoo hufaa kwa mavazi yako; Na mbuzi ni thamani ya shamba Tena yatakuwapo maziwa ya mbuzi, Ya kukutosha kwa chakula chako, Na chakula cha watu wa nyumbani mwako, Na posho la vijakazi vyako.