Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mit 26:3-12

Mit 26:3-12 SUV

Mjeledi kwa farasi, lijamu kwa punda, Na fimbo kwa mgongo wa mpumbavu. Usimjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake; Usije ukafanana naye. Umjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake; Asije akawa mwenye hekima machoni pake. Apelekaye ujumbe kwa mkono wa mpumbavu Hujikata miguu, na kunywa hasara. Miguu yake achechemeaye huwa dhaifu; Kadhalika mithali katika kinywa cha mpumbavu. Kama mfuko wa vito katika chungu ya mawe; Kadhalika mtu amheshimuye mpumbavu. Kama mwiba uingiao katika mkono wa mlevi; Kadhalika mithali katika kinywa cha mpumbavu. Fundi stadi hufanyiza vitu vyote; Bali amwajiriye mpumbavu ni kama awaajiriye watu wapitao. Kama vile mbwa arudiavyo matapiko yake; Kadhalika mpumbavu afanya upumbavu tena. Je! Wamwona mtu mwenye hekima machoni pake mwenyewe? Afadhali kumtumaini mpumbavu kuliko yeye.

Soma Mit 26