Mit 23:1-9
Mit 23:1-9 SUV
Utakapoketi kwa chakula pamoja na mtawala, Mwangalie sana yeye aliye mbele yako. Tena ujitie kisu kooni, Kama ukiwa mlafi. Usivitamani vyakula vyake vya anasa; Kwa maana ni vyakula vya hila. Usijitaabishe ili kupata utajiri; Acha kuzitegemea akili zako mwenyewe. Je! Utavikazia macho vile ambavyo si kitu? Maana bila shaka mali hujifanyia mabawa, Kama tai arukaye mbinguni. Usile mkate wa mtu mwenye husuda; Wala usivitamani vyakula vyake vya anasa; Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo. Akuambia, Haya, kula, kunywa; Lakini moyo wake hauwi pamoja nawe. Tonge lile ulilokula utalitapika, Na maneno yako matamu yatakupotea. Usiseme masikioni mwa mpumbavu; Maana atadharau hekima ya maneno yako.